Mauzo ya soko la awali ni njia kuu ya masoko ya kahawa ambapo kahawa huuzwa baada ya kufanyiwa hatua ya kwanza ya usindikaji kwa ajili ya kuongeza thamani.
Chini ya tawi hili la mauzo, kahawa huuzwa katika mfumo wa graiki kwa kahawa zilizosafishwa na michanjo kavu kwa kahawa zisizosafishwa.
Wakulima wanaweza kuchagua kuuza kahawa zao kwa wanunuzi binafsi wenye leseni au kuwasilisha kwa vyama vyao vya ushirika kufanya biashara kwa niaba yao.