Ukaangaji wa Kahawa

Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) kupitia Kitengo cha Ukaangaji Kahawa (Coffee Roasting Unit – CRU) kinatoa huduma za ukaangaji na usagaji kahawa kwa gharama nafuu. Kupitia kitengo hiki, kahawa ya TanCafe huandaliwa na kusambazwa kwa wateja mbalimbali ndani na nje ya nchi. Bidhaa zinazopatikana chini ya chapa ya TanCafe ni pamoja na TanCafe Kilele, TanCafe Twiga na TanCafe Ghahawa.

CRU pia kinatekeleza jukumu la kuongeza thamani ya kahawa ya Tanzania kwa kutoa mafunzo ya vitendo kwa wakulima, vikundi vya ushirika na wajasiriamali wadogo.

Kupitia maabara zake, CRU hutoa mafunzo ya ubora wa kahawa kuanzia hatua ya ukaangaji, usagaji na uandaaji wa vinywaji vya kahawa. Vilevile, kitengo hiki hutoa huduma za ushauri kwa wawekezaji na wasindikaji juu ya viwango bora vya ukaangaji vinavyokidhi mahitaji ya soko la zitaifa na kimataifa.

Lengo kuu la CRU ni kuhakikisha kahawa ya Tanzania, hususan chapa ya TanCafe na bidhaa zake kuu (Kilele, Twiga na Ghahawa), inaendelea kuwa na ushindani mkubwa katika masoko ya kikanda na ya kimataifa kupitia ubora na ongezeko la thamani.