TAARIFA KWA UMMA
KUANZA KWA MINADA YA KAHAWA MKOANI KAGERA TAREHE 04/06/2024
Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) inawatangazia wadau wote wa kahawa kuwa itaendesha mnada wa kwanza wa kahawa Mkoani Kagera siku ya Jumanne tarehe 04/06/2024 kuanzia saa 05:00 asubuhi.
Mnada huu utafanyika kwa njia ya mtandao (Online) ambapo wanunuzi wenye leseni wataweza kushiriki wakiwa sehemu yoyote ndani ya Tanzania na pia kushiriki mnada kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. Pia wadau wengine wanaruhusiwa na wanaweza kufuatilia mwenendo wa mnada huo katika ukumbi huo.
Aidha, Bodi inawataka wanunuzi wenye leseni na wenye nia ya kushiriki katika minada kuweka amana ya Shilingi Milioni 10 kwenye akaunti ya Bodi OlJ1038896702 Iliyoko CRDB Bank (Jina Tanzania Coffee Board) pamoja na kutekeleza matakwa mengine kama ilivyoelekezwa katika mwongozo No. 1 wa usimamizi wa masoko ya kahawa kwa msimu wa 2024/2025.
Kabrasha la mnada (Sales Catalogue) litapatikana katika tovuti ya Bodi ya Kahawa www.coffeeboard-or-tz pamoja na kutumwa kwenye barua pepe za wanunuzi,
Wanunuzi watakaohttaji msaada zaidi wawasiliane nasi kupitia namba 0778024368, 0752360225 na 0754289167-
F.J. Nyarusi
Kny: MKURUGENZI MKUU