JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KILIMO
BODI YA KAHAWA TANZANIA
TANGAZO
MABADILIKO YA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA 14 WA WADAU WA KAHAWA NCHINI
Taarifa inatolewa kwamba kutokana na sababu zisizozuilika kumekuwa na mabadiliko ya tarehe ya Mkutano Mkuu wa kumi na Nne (14) wa wadau wa kahawa uliopangwa kufanyika tarehe 17 Aprili, 2024. Mkutano huo sasa utafanyika tarehe 16 Aprili, 2024 katika Hoteli ya Morena Jijini Dodoma. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb).
Bodi ya Kahawa inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kuhusiana na mabadiliko haya.
Mambo mengine kuhusiana na mkutano huo yanabaki kama ilivyotangazwa awali.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Primus O. Kimaryo
Mkurugenzi Mkuu
Bodi ya Kahawa Tanzania
S. L. P. 732 – Moshi, Simu: 027-2752324
Barua pepe: info@coffee.go.tz; Tovuti: www.coffee.go.tz