Imewekwa: 21 Feb, 2023
Mkutano Mkuu wa 11 waBodi ya Kahawa Tanzania

Bodi ya Kahawa Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo ilifanya Kongamano la Wadau wa zao la Kahawa tarehe 17 Juni, 2021 na kufuatiwa na Mkutano wa 11 wa Wadau wa zao la Kahawa tarehe 18 Juni, 2021 katika ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Prof. Adolf F. Mkenda (Mb) Waziri wa Kilimo. Mkutano huo uligharamiwa na Bodi ya Kahawa kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwa ni pamoja na:

Taasisi ya ANSAF, Benki ya NMB, Solidaridad, Café Africa, Benki ya CRDB, Dormans, Tanzania Coffee Stakeholders, Benki ya NBC, ED&F MAN, DAE, Coffee Management experts, Mbinga Coffee, Ibero, Cotacof, Kijani Hai Tanzania, City Coffee Limited, Benki ya Stanbic na Mambo Coffee Co. Mkutano huu ulifanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 54 ya Kanuni za Kahawa 2013.

Mkutano huu ni wa kumi na moja kufanyika tangu mikutano ya wadau wa mazao makuu ya biashara yanayosimamiwa na Bodi za Mazao kutambulika kisheria. Mikutano hii inatoa fursa kwa wadau wa mazao hayo, pamoja na mambo mengine, kutoa michango yao kuhusu utekelezaji wa mikakati na mipango mbalimbali ya uendelezaji wa mazao husika. Wajumbe waliohudhuria mkutano huo wameorodheshwa katika Kiambatisho Na.1