Imewekwa: 18 Jul, 2025
JAMII YAHAMASISHWA KUENDELEA KUNYWA KAHAWA

Bodi ya Kahawa Tanzania(TCB) imeendelea kuhamasisha jamii kuhusu unywaji wa kahawa,hamasa hiyo imetolewa katika uzinduzi wa kampeni ya Wapanda mlima na waendesha baiskeli wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangia wagonjwa wa Maambukizi ya VVU (GGM kili Challenge) inayoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na serikali chini ya Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa, Afisa usimamizi ubora wa kahawa Bi. Annastazia Shirima, Amesema Bodi imejiwekea lengo la kuongeza Unywaji wa kahawa ili kufikia asilimia 15 ya kahawa yote inayozalishwa nchini.

Wapanda Mlima hao wanatarajiwa kushuka kileleni ifikapo Julai 24 mwaka huu ambapo watapokelewa katika geti la Mweka.