
BODI ya Kahawa Tanzania, imeendelea kuhamasisha jamii kuhusu unywaji kahawa.
Hamasa hiyo imetolewa leo katika uzinduzi wa Kampeni ya wapanda mlima na waendesha baiskeli wa Mlima Kilimanjaro.
Uzinduzi wa kampeni hiyo iliyolenga kupambana na kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini, umefanyika katika geti la Machame.
Akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa katika hafla hiyo, afisa usimamizi ubora wa Bodi ya Kahawa, Anastasia Shirima, amesema bodi imejiwekea lengo la kuongeza unywaji wa kahawa ili kufikia asilimia 15 ya kahawa yote inayozalishwa nchini.
Wapanda Mlima hao wanatarajiwa kushuka kileleni ifikapo Julai 25, mwaka huu, ambapo watapokelewa katika geti la Mweka.