
MKUTANO MKUU WA KUMI NA TANO (15) WA WADAU WA KAHAWA
Mkutano Mkuu wa kumi na tano (15) wa wadau wa kahawa unatarajiwa kufanyika tarehe 3 mpaka 4 Julai 2025 kuanzia saa 2:30 Asubuhi katika ukumbi wa Vicent uliopo St. Gaspar Hotel and Conference Center Jijini Dodoma.
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb). Mkutano huu unafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 54(1) ya Kanuni ya Tasnia ya Kahawa 2013 na unatarajiwa Pamoja na mambo mengine kujadili dondoo zifuatazo.
- Kufungua Mkutano.
- Kuridhia dondoo za mkutano.
- Kupokea Taarifa na kujadili utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano Mkuu wa kumi na Nne(14) wa wadau wa Kahawa uliofanyika Aprili, 2024.
- Kupokea na kujadili hali ya Tasnia ya Kahawa Nchini.
- Kupokea na kujadili taarifa ya makusanyo ya michango ya fedha za maendereo ya zao.
- Kupokea taarifa ya sekta ya Kahawa katika kutekeleza matakwa ya sheria ya kuzuia uharibifu wa misitu ya Jumuiya ya Ulaya (EUDR).
- Kupokea taarifa ya maandalizi ya mfuko wa mbolea kwa wakulima wa kahawa.
- Kujadili na kukubaliana maazimio ya Mkutano wa 15 wa wadau wa kahawa.
- Kufunga Mkutano.
Maelezo
Washiriki wa mkutano huu wameainishwa katika kanuni za Tasnia ya Kahawa 2013 na watatumiwa mialiko rasmi.