Imewekwa: 18 Dec, 2025
Washindi wa mashindano ya Kahawa Bora Tanzania kwa mwaka wa 2025-26

Washindi wa mashindano ya Kahawa Bora Tanzania kwa mwaka wa 2025-26 wamepokea tuzo na vyeti vyao katika hafla ya kipekee iliyofanyika tarehe 28 Novemba katika mkoa wa Mbeya. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa.

Shindano hili limeonyesha umahiri wa wakulima na wazalishaji wa kahawa kutoka mikoa yote ya uzalishaji nchini. Mhe. Itunda, akizungumza kwenye tukio hilo, aliwapongeza washindi pamoja na wakulima wote waliochangia katika kuimarisha ubora wa kahawa ya Tanzania. “Jitihada zenu zinaendelea kuinua hadhi ya kahawa yetu katika soko la kimataifa na kuonyesha ubora wa zao hili muhimu,” alisema Mhe. Itunda.

Idadi kamili ya washindi kwa kila kundi ilitangazwa rasmi, na washindi walipewa tuzo pamoja na vyeti vya kutambua mchango wao katika sekta ya kahawa. Tukio hilo lilikuwa fursa ya kuhimiza ushindani wa kiubora na kuongeza motisha kwa wakulima wote kuendeleza uzalishaji wa kahawa ya kiwango cha juu.

Mashindano ya Kahawa Bora Tanzania yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuthamini juhudi za wakulima na kutangaza ubora wa kahawa ya nchi yetu katika soko la kimataifa.

 

Bofya link hapa chini kupata;

Orodha ya Washindi wa Kahawa Bora Tanzania 2025-26