15 Apr, 2024 08:30 AM Morena Hotel, Dodoma - Tanzania

Mkutano Mkuu wa kumi na nne (14) wa wadau wa kahawa unatarajiwa kufanyika tarehe 16 Aprili, 2024 kuanzia saa 2.30 Asubuhi katika ukumbi wa Hoteli ya Morena Jijini Dodoma. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb). Mkutano huu unafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 54(1) ya Kanuni za tasnia ya Kahawa 2013 na unatarajiwa pamoja mambo mengine kujadili dondoo zifuatazo:

  1. Kufungua mkutano.
  2. Kuchagua mwenyekiti wa mkutano
  3. Kuridhia dondoo za mkutano.
  4. Kupokea taarifa na kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa kumi na tatu (13) wa wadau wa kahawa uliofanyika Juni, 2023.
  5. Kupokea na kujadili hali ya tasnia ya kahawa nchini.
  6. Kupokea na kujadili taarifa ya makusanyo ya michango ya fedha za maendeleo ya zao.
  7. Kupokea taarifa ya maandalizi ya mfuko wa mbolea kwa wakulima wa Kahawa. 
  8. Kujadili na kukubaliana maazimio ya mkutano wa 14 wa wadau wa kahawa.
  9. Kufunga mkutano.

Maelezo

  1. Washiriki wa mkutano huu wameainishwa katika Kanuni za Tasnia ya Kahawa 2013 na watatumiwa mialiko rasmi.
  2. Mkutano huu unagharamiwa na wadau wa kahawa kwa umoja wao.

 

MKUTANO MKUU WA 14 WA WADAU WA KAHAWA