01 Jun, 2026
08:00AM - 04:00PM
St. Gaspar Hotel and Conference, Dodoma
Mkutano Mkuu wa kumi na sita (16) wa wadau wa kahawa unatarajiwa kufanyika tarehe 4 mpaka 5 Juni 2026 kuanzia saa 2:30 Asubuhi katika ukumbi wa Vicent uliopo St. Gaspar Hotel and Conference Center Jijini Dodoma.
Mkutano huu unafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 54(1) ya Kanuni za tasnia ya Kahawa 2013 na unatarajiwa pamoja na mambo mengine kujadili dondoo zifuatazo;
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo (Mb).Mkutano huu unafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 54(1) ya Kanuni ya Tasnia ya Kahawa 2013 na unatarajiwa Pamoja na mambo mengine kujadili dondoo zifuatazo.
- Kufungua mkutano.
- Kuridhia dondoo za mkutano.
- Kupokea taarifa na kujadili utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa kumi na tano (15) wa wadau wa kahawa uliofanyika Julai, 2025.
- Kupokea na kujadili hali ya tasnia ya kahawa nchini.
- Kupokea na kujadili taarifa ya makusanyo ya michango ya fedha za maendeleo ya zao.
- Kupokea taarifa ya maendeleo ya sekta ya kahawa katika maandalizi ya kutekeleza matakwa ya kanuni ya kuzuia uharibifu wa misitu ya Jumuiya ya Ulaya (EUDR).
- Kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kanzidata na usajili wa wakulima wa kahawa.
- Kujadili na kukubaliana maazimio ya Mkutano wa 16 wa Wadau wa Kahawa.
- Kufunga mkutano.
Maelezo
Washiriki wa mkutano huu wameainishwa katika Kanuni za Tasnia ya Kahawa 2013 na watatumwa mialiko rasmi.

