Imewekwa: 06 Mar, 2026
TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA WA KAHAWA NA MAZAO MENGINE

Bodi ya Kahawa (TCB), tawi la Tanga linapenda kuwataarifu wafanyabiashara wote wa kahawa na mazao mengine ya biashara kuhusu uwepo wa maghala ya kisasa ya kuhifadhi mazao yaliyo karibu na Bandari ya Tanga.

Maghala haya yanapatikana katika eneo la Gofu Viwandani, takribani dakika tano kutoka bandari ya Tanga. Yameandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuhifadhi mazao kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi au kuingizwa nchini kupitia bandari hiyo.

Kila ghala lina uwezo wa kuhifadhi hadi tani 5,000 za mazao, hususani zao la kahawa. Aidha, maghala haya yana mifumo madhubuti ya ulinzi na usalama pamoja na huduma za uhakika, hivyo kuhakikisha mazao ya wafanyabiashara yanahifadhiwa katika mazingira salama na yanayozingatia ubora unaotakiwa.

Huduma zinazotolewa katika maghala haya zinatumia teknolojia ya kisasa, na zinajumuisha:

  • Kuandaa na kupanga kahawa kwa ajili ya usafirishaji.
  • Kupakia na kuhifadhi mazao kwa usalama.
  • Kuratibu taratibu za usafirishaji wa mizigo kwenda nje ya nchi pamoja na huduma za uondoaji mizigo bandarini(Clearing and Forwarding)

Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) inawahimiza wafanyabiashara wa kahawa na mazao mengine kutumia fursa ya huduma hizi ili kurahisisha uhifadhi na usafirishaji wa mazao yao kupitia Bandari ya Tanga.

Kwa mawasiliano zaidi.
Simu: 0656 045 958