Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amezindua Migahawa ya Kahawa inayotembea ikiwa ni mkakati wa kuongeza ushiriki wa vijana katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kahawa nchini.
Mhe. Majaliwa amezindua migahawa hiyo leo katika hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane, yanayofanyika kitaifa kwenye Viwanja vya Nzuguni, Dodoma Mjini.
Waziri Mkuu ametoa pongezi kwa Wizara ya kilimo pamoja na Bodi ya Kahawa kwa kufanya ubunifu wa mradi huo ambao utakuwa chachu ya ongezeko la ajira nchini hususan kwa vijana.
Migahawa hiyo ya Kahawa inayotembea, itasimamiwa na Bodi ya Kahawa Tanzania kupitia Mradi wa Jenga Kesho iliyo bora (BBT) ambao upo chini ya Wizara ya Kilimo.